.

.

.

.

Friday, November 27, 2015

TRA KAZINI

MAMLAKA ya Mapato
Tanzania(TRA), imeanza
operesheni maalumu ya
kunasa wafanyabishara wakubwa
ambao wengine ni wadaiwa sugu
ambapo wanadaiwa na mamlaka hiyo
huku wafanyabishara wa duka la simu
la Sapna lililopo eneo la Posta mpya
jijini Dar es Salaam likitiwa kufuli.
Operesheni ya TRA dhidi ya
wanaodaiwa fedha ilianza jana maeneo
mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam
ambapo maofisa wa mamlaka hiyo
walikuwa wanakwenda eneo moja hadi
jingine na kote ambako wamekwenda
wamefunga ofisi za wafanyabishara
hao.
Maofisa wa TRA waliokuwa
na nyaraka mbalimbali za madeni
walipokuwa wanafika kwenye maeneo
ya wafanyabishara hao hawakuwa na
muda wa kupoteza zaidi ya kufunga
ofisi huku baadhi ya maofisa hao
walikuwa wakisema kuwa Hapa Kazi
Tu.
Duka la Sapna ililifungwa jana saa
tisa alasiri ambapo maofisa wa TRA
ambao hawakuwa tayari kutaja majina
yao walidai kuwa wamiliki wa duka
hilo ni miongoni mwa wanaodaiwa
na TRA na tena ni kiasi kikubwa cha
fedha.Hata hivyo hawakutaja kiwango
halisi cha fedha huku wakifafanua kuwa
wamiliki wa duka hilo walipewa taarifa
mapema, hivyo hawakuvamia zaidi ya
kutumia utaratibu maalumu.
Wakati duka hilo linafungwa
wananchi walikuwa eneo hilo
walijikuta wakishangaa kuona namna
ambavyo wamiliki wa duka hilo wenye
asili ya Asia wakibaki wameshika
vichwa bila kujua la kufanya.Moafisa
wa TRA mbali ya kufunga duka hilo,
pia waliamua kufunga gari la mmoja
wa wamiliki wa duka hilo.
Mbali ya kufunga duka hilo pia
maofisa wa TRA walikwenda kwenye
ofisi za Shirika la Usari Dar es Salaam
(UDA), ambako nako wamekamata
baadhi ya magari kutokana na kudaiwa
kodi huku pia ikielezwa eneo lingine
ambalo mamlaka hiyo imefanya
operesheni ni eneo la Victoria ambapo
kuna kampuni inayohusika na uuzaji
wa redio upepo na rimoti za magari
.Kwenye eneo hilo magari manne
yamechukuliwa na TRA.
Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa
wa TRA ni kwamba operesheni
hiyo itaendelea tena leo huku pia
ikielezwa kuna viwanda mbalimbali
ambavyo vimefungwa kwa kushindwa
kulipa kodi.Hata hivyo alipotafutwa
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
mlipa kodi TRA Richard Kayombo
kuzungumzia operesheni hiyo

hakupatikana.

No comments:

Post a Comment