.

.

.

.

Thursday, September 10, 2015

KIDUME KIPYA CHA AMBER ROSE

MAIN-Amber-Rose-has-a-new-man-Odell-Beckham-JrAmber Rose atoka na Mwanamichezo Odell Beckham Jr.
New-York-Giants-wide-receiver-Odell-Beckham-Jr-attends-China-Through-the-Looking-Glass-the-2015-Costume-Institute-Gala
Mwanamichezo Odell Beckham Jr
 Celebrity-arrivals-at-The-Fresh-Air-Fund-Annual-Spring-Gala-in-NYCPictured-Odell-Beckham-Jr

INAONEKANA mwanamitindo nyota wa Marekani, Amber Rose (31), ameachana moja kwa moja na mumewe, Wiz Khalifa, kwani inasemekana mrembo huyo ameanza uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa timu ya New York Giants, Odell Beckham Jr. (22).
Vyanzo mbalimbali vinasema, mwanariadha huyo amekuwa akimfuatilia mrembo huyo kwa miezi kadhaa kabla ya kumpata kupitia rafiki yake na hatimaye kutoka naye katika matukio kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuonekana ‘wakila bata’ kwenye mgahawa wa TAO jijini New York mwezi uliopita.
Pia habari zimesema Odell alimshangaza Amber kwa kumpa kitita cha maua ambayo ni alama ya upendo.  Hii ni mbali na kuonyesha upendo wake kwa Amber katika mtandao wa Twitter alipoandika maneno kuhusu penzi la hilo.
Amber alianza kutoka na rapa, Wiz, mapema mwaka 2011 kabla hawajachumbiana mnamo Machi 2012 na baadaye kufunga ndoa mwaka uliofuata na kumpata mtoto wa kiume aitwaye Sebastian Taylor, Februari
21, 2013.
Septemba 2014 Amber alifungua kesi kuomba talaka dhidi ya rapa huyo akidai ni kutokana na mambo ambayo hayawezi kusuluhishwa.

No comments:

Post a Comment