.

.

.

.

Friday, April 24, 2015

ALHAJI ALIKO DANGOTE ATEMBELEA MTWARA VIJIJINI


 Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dangote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.

PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Alhaji Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza kujenga bbandari hiyo mapema mwaka huu.
 Msafara wa Alhaji Dangote ukitoka eneo atakalojenga bandari katika Kijiji cha Mgao
 Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.
 Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti


 Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote
 Alhaji Dangote akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (kushoto) Mwakilishi wake hapa nchini, Esther Baruti na Balozi Dk, Majanbu

 
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote  eneo la ujenzi wa Bandari
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa  na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
 Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari


 Alhaji Dangote akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo

 Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa





 Alhaji akijadiliana jambo na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji, Kushoto ni Paschasia Ngaiza Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais wa Tanzania, Premy Kibanga ambaye pia alikuwepo kwenye ziara hiyo.

 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimuaga Alhaji Dangote uwanjani hapo
 Alhaji Dangote akiteta jambo na mwakilishi wake hapa nchini, Esther muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Ethiopia na hatimaye Lagos, Nigeria.
 Alhaji Dangote akiaga

 
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote na ujumbe wake ikiondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara

No comments:

Post a Comment